Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 31 Januari 2016 04:30

Saudia inawalenga raia vitani nchini Yemen

Saudia inawalenga raia vitani nchini Yemen
Afisa mmoja wa ngazi za juu wa Jumuiya ya Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) amesema kuwa, wanajeshi wa Saudi Arabia wamekuwa wakiwalenga raia katika mashambulio yao huko nchini Yemen.

Jason Cone, Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) nchini Marekani ameandika makala katika mtandao wa gazeti la Times kwamba, katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, ndege za kijeshi za Saudi Arabia zimeshambulia vituo vitatu vya tiba vinavyosimamiwa na jumuiya hiyo. Afisa huyo wa Jumuiya ya Madaktari Wasio na Mipaka ameongeza kuwa, inaonekana kuwa, kuwalenga raia na miundo mbinu ya Yemen ni katika malengo ya vikosi vya Saudia huko Yemen.

Jason Cone ameashiria pia mashambulio ya anga ya Saudia huko Yemen dhidi ya taasisi hiyo ya utoaji misaada ya kibinadamu. Amesema, masuala yote hayo yanabainisha na kuweka wazi ukiukaji wa wazi kabisa wa sheria za vita na kinga ya kisheria ya taasisi na wafanyakazi wa masuala ya kitiba.

Saudia na waitifaki wake waliivamia Yemen mwezi Machi mwaka uliopita na takwimu zinaonyesha kuwa hadi sasa karibu watu elfu kumi wameuawa na maelfu ya wengine wamejeruhiwa huku makumi ya maelfu ya wengine wakiachwa bila makazi. Wengi wa wahanga wa hujuma za Saudi Arabia nchini Yemen ni wanawake na watoto wadogo.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)