Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 30 Januari 2016 05:11

Ansarullah: Wasaudi wameingiwa na kiwewe

Ansarullah: Wasaudi wameingiwa na kiwewe

Msemaji wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kukatwa urushaji matangazo ya kanali ya televisheni ya al-Maseera katika satalaiti ya Nile Sat ni ishara ya wahka na kiwewe kilichowapata watawala wa Aal Saud.

Muhammad Abdussalam ametoa taarifa akiashiria hatua ya kuzuiliwa kurushwa matangazo ya kanali ya televisheni ya Yemen ya al-Maseera katika satalaiti ya Nile Sat na kueleza kwamba wavamizi wa Kisaudi wameshindwa kuvumilia uwepo wa kanali ya al-Maseera, japokuwa wao wenyewe wana vyombo chungu nzima vya habari vinavyoeneza uongo kitaalamu kwa maslahi yao.

Msemaji wa Ansarullah ameongeza kuwa kanali ya televisheni ya al-Maseera inasaidia kubainisha ukweli wa yanayojiri kwenye medani za vita na machungu na mateso wanayopata watu kutokana na uvamizi wa kidhalimu na mzingiro wa kinyama wa Saudia dhidi ya wananchi wa Yemen; lakini suala hilo limewatia kiwewe Wasaudi.

Utawala wa kifalme wa ukoo wa Aal Saud nchini Saudi Arabia umayewekea mashinikizo mashirika ya Nile Sat na Arab Sat na kupelekea kukatwa urushaji wa matangazo ya kanali ya televisheni ya al-Maseera ya Yemen na al-Luuluu ya Bahrain katika satalaiti ya Nile Sat na kanali za al-Mayadeen na al-Manaar za Lebanon katika satalaiti ya Arab Sat.../

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)