Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 23 Januari 2016 11:40

Askari kadhaa wa Saudia waangamizwa nchini Yemen

Askari kadhaa wa Saudia waangamizwa nchini Yemen
Askari kadhaa wa Saudia wameuawa katika mashambulizi ya jeshi la Yemen kwa kushirikiana na harakati ya wananchi ya Ansarullah huko kusini mwa nchi hiyo.

Askari hao wa Saudia wameuawa wakati jeshi la Yemen kwa kushirikiana na harakati ya wananchi ya Ansarullah liliposhambulia kwa makombora kambi ya jeshi la Saudia ya al-Tuwaal katika mji wa mpakani wa Jizani. Aidha jeshi la Yemen limeshambulia askari wa Saudia katika eneo la al-Mut'in na kusini mwa mji wa al-Khubah, na kuua askari kashaa wa nchi hiyo. Inaelezwa kuwa, katika mashambulizi hayo mbali na kuua askari kadhaa wa Saudia, jeshi la Yemen limeharibu vifaru na magari ya kijeshi yaliyokuwa yakitumiwa na askari hao. Mashambulizi ya Saudia nchini Yemen yalianza mwanzoni mwa mwaka uliopita 2015 kwa lengo la kuwalazimisha wananchi wa Yemen wamkubali rais aliyejiuzulu na kutoroka nchini humo, Abd Rabb Mansou Hadi.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)