Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 22 Januari 2016 10:32

Ndege za Israel, US, UK zaisadia Saudia kuhujumu Yemen

Ndege za Israel, US, UK zaisadia Saudia kuhujumu Yemen

Ndege za kivita za utawala haramu wa Israel, Marekani na Uingereza zinaisaidia Saudi Arabia kudondosha mabaomu huko Yemen, amefichua msemaji wa jeshi la Yemen.

Brigedia Jenerali Sharaf Luqman, msemaji wa Jeshi la Yemen amesema Alhamisi kuwa, kuna ushahidi kuwa ndege za kivita za Israel, Marekani na Uingereza ndizo ambazo zimekuwa zikidondosha mabomu kwa niaba ya Saudia nchini Yemen kwani marubani Wasaudi hawana uwezo wa kutumia ndege za kisasa zinazotumiwa kuangamiza Yemen. Afisa huyo wa kijeshi amesema hadi sasa wanajeshi wa Yemen na wapiganaji wa Harakati ya Ansarullah wamefanikiwa kuangusha ndege tatu za kivita aina ya F-16, helikopta 10 za kivita aina ya Apache na makumi ya ndege za kijasusi zisizo na rubani (surveillance drone).

Brigedia Jenerali Luqman ameongeza kuwa kuna wanajeshi mamluki 400 kutoka nchi za Ulaya na Amerika ya Latini hasa Colombia ambayo wameajiriwa na Saudia kushiriki katika vita vya Yemen. Uingereza na Marekani aidha zimekuwa zikipatia Saudia taarifa za kijasusi na ushauri wa kijeshi ili kufanikisha hujuma dhidi ya watu wa Yemen. Saudi Arabia imekuwa ikiishambulia Yemen kwa muda wa miezi 10 sasa ambapo watu 8,300 wameuawa, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto. Saudia inataka kuiondoa madarakani harakati ya Ansarullah na kumrejesha kibaraka wake rais aliyejiuzulu na kuitoroka nchi, Abdu Rabuh Mansour Hadi.

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)