Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 20 Januari 2016 11:07

Saudia yashambulia maeneo ya mji mkuu wa Yemen

Saudia yashambulia maeneo ya mji mkuu wa Yemen

Ndege za kivita za Saudi Arabia zimeishambulia miji ya Sana'a na Maarib nchini Yemen.

Televisheni ya al Masira imeripoti kuwa, ndege za kivita za utawala vamizi wa Aal Saud leo asubuhi zimefanya mashambulizi kadhaa kaskazini mwa Sana'a mji mkuu wa Yemen na hadi kufikia sasa hakuna taarifa yoyote iliyotolewa kuhusu maafa yaliyosababishwa na mashambulizi hayo.

Ndege za kivita za Saudi Arabia jana usiku pia zilifanya mashambulio kumi na tano katika maeneo tofauti ya mkoa wa Ma'rib katikati mwa Yemen na kubomoa maduka na shule na vituo kadhaa vya usalama.

Saudi Arabia ilianzisha uvamizi wa kijeshi huko Yemen tangu mwanzoni mwa mwaka jana chini ya muungano unaozishirikisha baadhi ya nchi za Kiarabu za eneo kwa kuungwa mkono na Marekani, lengo kuu likiwa ni kumrejesha madarakani Rais wa nchi hiyo aliyejiuzulu Abd Rabu Mansour Hadi na ili kuwazuia kushika madaraka wanamapinduzi wa nchi hiyo ambao wanadhamini usalama wa miji ya nchi hiyo. Maelfu ya Wayemeni wakiwemo wanawake na watoto wameuliwa na kujeruhiwa na makumi ya maelfu wamekuwa wakimbizi kutokana na mashambulizi ya kijeshi ya Saudi Arabia na waitifaki wake. Mbali na hayo, asilimia 80 ya miundombinu, huduma za kijamii na kitiba zimeharibiwa na kubomolewa katika uvamizi huo wa kijeshi wa utawala wa Aal Saud dhidi ya Yemen.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)