Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 16 Januari 2016 20:04

Saudi Arabia inatumia mabomu ya vishada Yemen

Saudi Arabia inatumia mabomu ya vishada Yemen

Shirika la Msamaha Duniani (Amnesty International) limetangaza kuwa muungano wa vita dhidi ya Yemen unaoongozwa na Saudi Arabia kwa mara nyingine tena umetumia mabomu ya vishada katika mashambulizi yake huko Yemen.

Shirika hilo limebainisha kuwa lina ushahidi wa kuthibitisha suala hilo. Amnesty International imeeleza kuwa imekusanya taarifa zinazoonyesha kuwa tarehe 6 mwezi huu, Saudia iliushambulia mji mkuu wa Yemen Sana'a kwa kutumia mabomu ya vishada.

Shirika la Msamaha Duniani limesema katika taarifa yake ya leo kuwa ndege za kivita za Saudi Arabia lililishambulia eneo la Ma'in huko Sana'a na kumuua mtoto mmoja na kuwajeruhi raia wengine sita. Shirika la Amnesty International lenye makao yake London, Uingereza limeongeza kuwa lilipata taarifa kupitia wenyeji wa eneo hilo, familia za watu waliouliwa, wanajeshi na waandishi wa habari kuhusu Saudi Arabia kutumia mabomu ya vishada katika mashambulizi yake huko Sana'a. Shirika hilo limesisitiza kuwa ni Saudia pekee ndiyo iliyo na uwezo wa kutumia mabomu hayo ya vishada na kwa sababu hiyo wanaitaka nchi hiyo kuacha kutumia aina hiyo ya mabomu.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)