Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 15 Januari 2016 06:40

Misri, Saudia zaongeza mkataba kuishambulia Yemen

Misri, Saudia zaongeza mkataba kuishambulia Yemen

Baraza la ulinzi la kitaifa nchini Misri, limerefusha mkataba na utawala wa Aal Saudi dhidi ya Yemen, katika vita vya kivamizi vinavyoongozwa na Saudia dhidi ya nchi hiyo ya Waislamu na Waarabu.

Taarifa iliyotolewa na ikulu ya Rais Abdel Fattah el-Sisi wa Misri imesema kuwa, baraza hilo la ulinzi wa taifa limerefusha mkataba huo kwa kipindi cha mwaka mmoja zaidi dhidi ya Yemen.

Aidha imedai kuwa, Misri imekubali kurefusha kipindi cha mkataba huo na Saudia kwa kile ilichodaio kuwa ni kwa ajili ya kulinda usalama wa Misri na wa nchi nyingine za Kiarabu katika eneo la Bahari Nyekundu na Bab-el-Mandeb.

Baadhi ya duru za ndani nchini Misri zimefichua kuwa, Cairo imekubali kuongeza mkataba huo baada ya kupokea kiwango kikubwa cha cha dola za Marekani kutoka kwa utawala wa kiimla wa Aal Saud wa Saudi Arabia.

Hii ni katika hali ambayo tangu kuanza mashambulizi ya Saudia na waitifaki wake dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi wa Yemen, zaidi ya watu 7000 wamekwishauawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa, katika nchi hiyo ya Kiarabu.

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)