Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 13 Januari 2016 04:59

Yemen: Jinai zinazofanywa na Saudia zichunguzwe

Yemen: Jinai zinazofanywa na Saudia zichunguzwe
Wizara ya Haki za Binadamu ya Yemen imetaka iundwe tume ya kutafuta ukweli ili kuchunguza jinai za utawala wa Aal Saud dhidi ya wananchi wa Yemen.

Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo imelitaka Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu ziunde kamati ya kimataifa ya kuchunguza silaha zilizopigwa marufuku ambazo zinatumiwa na Saudia katika vita dhidi ya Yemen.

Huku ikiashiria mabomu ya vishada yaliyotumiwa na ukoo wa Aal Saud katika mikoa mbalimbali ya Yemen, taarifa hiyo imeissitiza kuwa Umoja wa Mataifa, nchi na jumuiya zote za kimataifa zinapaswa kuchukua hatua za haraka na za lazima ili kusimamisha mashambulio ya anga ya Saudia na waitifaki wake dhidi ya Yemen kulingana na hati ya Umoja wa Mataifa mikataba ya haki za binadamu.

Wizara ya Haki za Binadamu ya Yemen vilevile imelaani mauaji ya makusudi ya raia wa nchi hiyo yanayofanywa na Saudia kwa kutumia silaha zilizopigwa marufuku na kusisitiza kuwa utawala wa Aal Saud unapaswa kufunguliwa mashtaka kutokana na jinai hizo.../

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)