Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 11 Januari 2016 07:19

"Jinai za Saudia zisitishwe kabla ya mazungumzo"

"Jinai za Saudia zisitishwe kabla ya mazungumzo"

Msemaji wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema: harakati hiyo haitoshiriki kwenye mazungumzo yoyote mapya kama yale yaliyotangulia yaliyofanyika nchini Uswisi kabla ya Saudia kusimamisha jinai na mashambulio yake dhidi ya nchi hiyo.

Muhammad Abdussalam ameiambia kanali ya televisheni ya al-Maseera kuwa katika mazungumzo ya Disemba mwaka uliopita yaliyofanyika nchini Uswisi ujumbe wa Saudia ulikwenda kwenye mazungumzo hayo kwa ajili ya mambo mawili tu, ambayo ni kuachiliwa huru mateka watano na kuondolewa mzingiro wa Taiz.

Msemaji wa Ansarullah amebainisha kuwa Wasaudi hawana hata mamlaka ya kuamua kuhusiana na uvamizi walioanzisha dhidi ya Yemen na kwamba uamuzi kuhusiana na uvamizi huo dhidi ya wananchi madhulumu wa Yemen uko mikononi mwa balozi wa Marekani mjini Sana'a.

Huku akiashiria kuwa Al-Qaeda na Daesh yamebuniwa na Marekani, Muhammad Abdussalam amesema, makundi hayo ya kigaidi yamepeperusha bendera zao juu ya majengo ya benki na taasisi za serikali katika mji wa Al-Mukalla, makao makuu ya mkoa wa Hadhramaut, lakini hayaandamwi na mashambulio ya ndege za kivita za Marekani.

Ameongeza kuwa Ansarullah inakutana na kufanya mazungumzo na makundi yote kwa uwazi na si katika mazingira ya faragha na kusisitiza kwamba wamesha waeleza bayana Wasaudi na Wamarekani kuwa wao ni wavamizi.

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)