Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 11 Januari 2016 06:20

Wanajeshi wa Saudia washambulia tena mji wa Qatif

Wanajeshi wa Saudia washambulia tena mji wa Qatif

Hatua za ukandamizaji za utawala wa Aal Saud dhidi ya wakazi wa mji wa Qatif, mashariki mwa Saudi Arabia zingali zinaendelea.

Televisheni ya al Manar ya nchini Lebanon imetangaza kuwa wanajeshi wa utawala wa Aal Saud kwa mara nyingine tena wamezishambulia nyumba za Waislamu wa Kishia wa mji wa Qatif mashariki mwa nchi hiyo. Wanajeshi hao wa Saudi Arabia wamezivamia nyumba za familia mbalimbali huko Qatif ambazo watu wake wamekuwa wakiandamana kwa amani kulalamikia kunyongwa mwanazuoni mkubwa Sheikh Nimr Baqir al Nimr.

Maeneo mbalimbali ya mashariki mwa Saudia yamekuwa yakishuhudia maandamano ya wananchi tangu tarehe Pili mwezi huu baada ya kutangazwa habari ya kunyongwa Sheikh Nimr na utawala wa Aal Saud.

Utawala wa Aal Saud tarehe Pili mwezi huu ulitangaza kumnyonga Sheikh Nimr Baqir al Nimr mwanazuoni mkubwa wa Kishia wa nchi hiyo. Hii ni katika hali ambayo makundi mbalimbali ya kisiasa, vyama na shakhsia kutoka maeneo tofauti duniani wamelaani kuuliwa shahidi Sheikh Baqir al Nimr kwa kosa la kupigania haki za kisheria za wananchi na ambazo zimeghusubiwa na ukoo wa Aal Saud. Hadi sasa kuna radiamali mbalimbali zinaendelea kutolewa kulaani mauaji hayo.

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)