Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 10 Januari 2016 19:21

Saudia yashambulia wagonjwa Yemen, yaua kadhaa

Saudia yashambulia wagonjwa Yemen, yaua kadhaa

Katika kuendelea na jinai zake huko Yemen, ndege za kivita za muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia zimeishambulia hospitali moja kaskazini mwa nchi hiyo.

Televisheni ya al Mayadeen ya nchini Lebanon imeripoti kuwa ndege za kivita za Saudia leo zimeipiga kwa makombora hospitali moja katika mkoa wa Sa'ada kaskazini mwa Yemen ambayo inaendeshwa na Jumuiya ya Madaktari wasio na Mipaka na kuuwa wagonjwa wasiopungua watano na kujeruhiwa wengine kumi.

Ndege za kivita za Saudi Arabia pia zimeyashambulia maeneo ya al Asdad na Marih katika mkoa wa Sa'ada na kuuwa raia kadhaa. Ndege za Saudia pia zimelishambulia soko moja katika mji wa Razih kwenye mkoa huo wa Sa'ada na kuuwa watu watatu na kujeruhi wengine watano.

Katika upande mwingine makundi ya kujitolea ya wananchi wa Yemen yamejibu jinai za Saudi Arabia kwa kufanya operesheni katika baadhi ya maeneo ya Jizan na Najran kusini mwa Saudia na kuwatia mbaroni wanajeshi kadhaa wa Saudi Arabia.

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)