Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Alkhamisi, 07 Januari 2016 04:33

Askari kadhaa wa Saudia waangamizwa Yemen

Askari kadhaa wa Saudia waangamizwa Yemen

Askari kadhaa wa Saudia wameangamizwa baada ya kushambuliwa na harakati ya wananchi nchini Yemen, wakati askari hao vibaraka walipokuwa wakijaribu kupenya na kuingia nchini humo.

Askari hao wa Saudia wameangamizwa leo na jeshi la Yemen kwa kushirikiana na harakati ya wananchi ya Answarullah, wakati vibaraka hao walipokuwa wakipenya katika kivuko cha al-Twawwal kilichopo kwenye mkoa wa Jizan ulio mwambao wa Bahari Nyekundu.

Mbali na askari wa Aal, Saud, magaidi kadhaa waliokuwa wakishirikiana na askari hao pia wameuawa.

Vilevile jeshi la Yemen likishirikiana na wapiganaji wa Ansarullah limedhibiti ngome kadhaa za vibaraka wa Saudia katika jimbo la Lahij, kusini mwa Yemen. Ngome hizo zilikuwa zikitumiwa na magaidi wa al-Qaida kwa ajili ya kushambulia maeneo tofauti ya Yemen ukiwemo mkoa wa Taiz, kusini mwa nchi hiyo.

Wakati huo huo jeshi la Yemen limesonga mbele kuelekea kambi ya kijeshi ya Labozah na kambi ya jeshi la anga ya al-Abd katika mkoa wa Lahij zilizokuwa zikidhibitiwa na vibaraka wa Saudia. Tayari maeneo ya al-Wazaiyah, al-Rahdah na Sharijah kusini mwa mkoa wa Lahij yamekombolewa na jeshi la Yemen na magaidi wa al-Qaida wamekimbia na kuacha zana na silaha mbalimbali za kivita.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)