Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 08 Mei 2015 12:28

Russia yaonya kutumwa vikosi vya nchi kavu Yemen

Russia yaonya kutumwa vikosi vya nchi kavu Yemen

Vitaly Churkin, mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa ameonya juu ya hatua yoyote ya kutumwa vikosi vya nchi kavu huko Yemen na kusema kuwa, hatua hiyo haitasaidia kumaliza mgogoro wa nchi hiyo. Amesema kuwa, kutumwa majeshi ya nchi kavu nchini Yemen, kutapelekea mgogoro huo kuwa mpana zaidi. Aidha mwakilishi huyo wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, anataraji kwamba makundi ya kisiasa nchini Yemen yataanza mchakato wa mazungumzo baina yao kwa upatanishi wa Umoja wa Mataifa ili kuupatia ufumbuzi mgogoro wa nchi yao. Amesema, mgogoro wa Yemen hauwezi kumalizika kwa mtutu wa bunduki wala mashambulizi ya ndege za kivita, bali unaweza kumalizika tu kwa njia ya mazungumzo. Aidha amesema kuwa Russia inataraji kuona usitishaji vita wa siku tano uliopendekezwa na Saudia utakuwa wa kudumu. Hivi karibuni mwakilishi huyo wa kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa alilaani vikali hatua ya nchi za Magharibi hasa Marekani na waitifaki wake ya kupuuza hali mbaya ya kibinaadamu nchini Yemen na wakati huo huo kujifanya kuwa wanaiunga mkono nchi hiyo. Churkin alisema hayo baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kushindwa kuunga mkono takwa la Russia la kusimamishwa vita haraka iwezekanavyo huko Yemen.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)