Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 11 Julai 2015 10:01

Siku ya Quds yaadhimishwa Kenya na Tanzania

Siku ya Quds yaadhimishwa Kenya na Tanzania

Kenya na Tanzania zilijiungana jana na mataifa mengine katika maadhimisho ya Siku ya
Kimataifa ya Quds. Waislamu jijini Nairobi waliadhimisha siku hiyo kwa
kufanya maandamano ya amani baada ya Swala ya Ijumaa katika mtaa wa Kibera, kiungani mwa mji mkuu wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki, huku wenzao wa nchini Tanzania wakishiriki maandamano hayo katika mikoa mbalimbali ya nchi hiyo.
Waandamanaji hao walisikika wakipiga nara za kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina, ambao ardhi yao imekaliwa kwa mabavu na utawala wa kizayuni wa Israel.

Jijini Nairobi, kilele cha maadhimisho hayo ilikua hotuba ya Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jijini Nairobi, Malek Hussein Givzad, ambaye amekosoa kimya cha jamii ya kimataifa mbele ya ukatili wanaofanyiwa Wapalestina. Amesema umoja na mshikamano miongoni mwa Waislamu ndio unaweza kuwa chachu kwa harakati ya kuilinda Quds tukufu, ambayo imekuwa ikikabiliwa na hujuma za wazayuni kila uchao.

Siku ya Kimataifa ya Quds huadhimishwa katika nchi nyingi za Kiislamu, katika Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhan kila mwaka. Jana mamilioni ya watu duniani waliandamana kote duniani kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Quds.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)