Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 10 Julai 2015 12:35

Miji 770 Iran yaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds

Miji 770  Iran yaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds

Ijumaa ya leo ya tarehe 10 Julai, ni Siku ya Kimataifa ya Quds. Waislamu na wapenda haki kote duniani wanaendelea na maandamano yao katika kona mbalimbali za dunia kuadhimisha siku hiyo muhimu ya kuliunga mkono taifa linalodhulumiwa la Palestina na Quds Tukufu.
Hapa nchini Iran, Baraza la Uratibu la Tablighi ya Kiislamu limetoa taarifa yake ya pili kwa mnasaba wa kuwadia Siku ya Kimataifa ya Quds na kusema kuwa, maandamano makubwa yameanza katika miji 770 ya Iran kuadhimisha siku hiyo.
Baraza hilo limesema, Siku ya Kimataifa ya Quds ni siku ya kutangaza ukombozi wa Palestina, kuunga mkono malengo matakatifu wa Palestina, kutangaza umma mkubwa wa Mtume Muhammad SAW kujibari na kujiweka kwao mbali na dhulma, ukatili na mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni, jinai za kundi la kigaidi la Daesh na makundi mengine ya kitakfiri.
Hadi tunaripoti habari hii, maandamano hayo yalikuwa yanaendelea katika miji 770 ya Iran na katika kona mbalimbali duniani huku waandamanaji wakiwa wamebeba mabango ya kulaani jinai za Israel na waitifaki wake.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)