Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Alkhamisi, 09 Julai 2015 23:02

Siku ya Kimataifa ya Quds kuadhimishwa kesho

Siku ya Kimataifa ya Quds kuadhimishwa kesho

Mamilioni ya wapenda haki kote ulimwenguni, kesho wataadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds. Kesho inasadifiana na Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ambayo ni Siku ya Kimataifa ya Quds ambapo wananchi wa Iran, Waislamu katika nchi nyingine na watetezi wa haki za binadamu kote duniani wataandamana wakionyesha mshikamano wao na wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina na kutangaza hasira na chuki zao dhidi ya utawala katili wa Israel unaoendelea kukalia kwa mabavu Quds Tukufu na kibla cha kwanza cha Waislamu. Viongozi mbalimbali wa kidini, kisiasa na kijamii wametoa wito kwa wapenda haki kote duniani kushiriki kwa wingi katika maandamano ya kesho ya Siku ya Kimataifa ya Quds na kupinga dhulma za Wazayuni wa Israel na waitifaki wao wa nchi za Magharibi hususan Marekani. Ni vyema kukumbusha hapa kuwa baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu hayati Ruhullah Khomeini aliitangaza Ijumaa ya mwisho ya kila mwezi wa Ramadhani kuwa siku ya Kimataifa ya Quds na kuwatetea wananchi wanaokandamizwa Wapalestina. Imam Khomein alisema: Nawaita Waislamu ulimwenguni kote kuadhimisha Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhan kama Siku ya Quds'na kutangaza mshikamano wa Waislamu katika kuunga mkono haki halisi za Waislamu wa Palestina.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)