Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Alkhamisi, 09 Julai 2015 10:00

Robert Turner: Israel inazuia kujengwa upya Ghaza

Robert Turner: Israel inazuia kujengwa upya Ghaza

Ijumaa ya kesho ya Julai 10 inatarajiwa kuwa Ijumaa ya mwisho ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani ambayo ni Siku ya Kimataifa ya Quds ya kuliunga mkono taifa linalodhulumiwa la Palestina.

Mamilioni ya Waislamu na wapenda haki kote duniani wanajiandaa kuadhimisha vilivyo siku hiyo katika hali ambayo, Umoja wa Mataifa umeutaka utawala wa Kizayuni wa Israel uache kuuzingira Ukanda wa Ghaza na kuruhusu kujengwa upya ukanda huo ulioharibiwa vibaya na mashambulizi ya kikati la Israel.

Robert Turner, mkurugenzi wa operesheni za shirika la Umoja wa Mataifa la UNRWA huko Ghaza amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea kuuzingira kila upande ukanda huo na hivyo kukwamisha juhudi zote za kuujenga upya.

Zaidi ya Wapalestina 2,500 waliuawa shahidi katika mashambulio ya mwaka jana ya Israel huko Ghaza huku zaidi ya mashahidi 500 kati ya Wapalestina hao wakiwa ni watoto wadogo. Makumi ya maelefu ya Wapalestina wengine wameharibiwa makazi yao na hadi hivi sasa wanaendelea kuteseka kutokana na eneo hilo kuzingirwa kila upande na utawala dhalimu wa Kizayuni.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)