Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 08 Julai 2015 20:16

Mataifa ya Waislamu yanafikisha kilio cha Wapalestina

Mataifa ya Waislamu yanafikisha kilio cha Wapalestina

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, mataifa ya Waislamu hususan taifa la Iran yanafikisha kwa walimwengu, kilio cha kudhulumiwa wananchi wa Palestina ambao wamefukuzwa kwenye nchi yao na utawala wa Kizayuni wa Israel, kwa miaka 66 sasa. Rais Hassan Rouhani amesema hayo alipohojiwa na mwandishi wa Radio Tehran kwa mnasaba wa kukaribisa Siku ya Kimataifa ya Quds ambayo ni Ijumaa ya mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Mwaka huu siku hiyo inasadifiana na Ijumaa ya keshokutwa ya Julai 10. Ameongeza kuwa, katika Siku ya Kimataifa ya Quds iliyotangazwa na Imam Khomeini MA, mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Waislamu kote duniani na hususan nchini Iran watawatangazia walimwengu dhulma wanayoendelea kufanyiwa Wapalestina na utawala wa Kizayuni na kwamba uchungu wa kukaliwa kwa mabavu ardhi hizo za Waislamu hauwezi kutoka katika nyoyo za Waislamu kote ulimwenguni. Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa, kwa hakika katika Siku ya Kimataifa ya Quds, umma wa Kiislamu unatangaza kwa sauti moja kwa walimwengu, dhulma wanayoendelea kufanyiwa ndugu zao wa Palestina na utawala dhalimu wa Kizayuni.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)