Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 07 Julai 2015 17:42

Siku ya Kimataifa ya Quds, ukumbusho wa Imam Khomeini

Siku ya Kimataifa ya Quds, ukumbusho wa Imam Khomeini

Mwanachama wa ngazi za juu wa Harakati ya Jihad al-Islami ya Palestina amesema kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds ni ukumbusho wa kudumu wa Imam Khomeini (MA).
Akizungumza leo na shirika la habari la Qudsna Marwan an-Najjar ameashiria msimamo imara wa Imam Khomeini (as) katika kutetea taifa la Palestina na kusema kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds ni nguzo kuu na ya kimsingi ya kutetea Quds Tukufu ambayo ilibuniwa na kuachwa nyuma na Imam Khomeini (MA). Amesema Siku ya Kimataifa ya Quds inawaletea fahari kubwa wapigania uhuru wote duniani na kwamba suala la Palestina si suala linalowahusu Wapalestina tu bali mataifa yote yanayotetea uhuru. Marwan an-Najjar ameashiria jinai zinazofanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Wapalestina na kusema bado Wapalestina wana moyo wa kudumisha mapambano yao dhidi ya maghasibu wa Kizayuni hadi pale watakaporejesha ardhi zao zinazokaliwa kwa mabavu na utawala wa Tel Aviv.
Kwa ufumbuzi wa Imam Khomeini (MA), mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kila mwaka Waislamu huadhimisha siku ya Quds kimataifa katika Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa madhumuni ya kutangaza mfungamano wao na mapambano ya watu wa Palestina dhidi ya uchokozi na ukandamizaji wa utawala haramu wa Israel.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)