Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 05 Julai 2015 14:29

Jannati: Siku ya Kimataifa ya Quds ni siku ya Uislamu

Jannati: Siku ya Kimataifa ya Quds ni siku ya Uislamu

Mkuu wa Baraza la Uratibu wa Tablighi ya Kiislamu la Iran amesema kuwa, Siku ya Kimataifa ya Quds ni siku ya Uislamu. Ayatullah Ahmad Jannati ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Kulinda Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa, Waislamu wanapaswa kusimama dhidi ya ubeberu wa dunia kwa nguvu zao zote katika Siku ya Kimataifa ya Quds.

Ayatullah Jannati amesema, Siku ya Kimataifa ya Quds ni siku ambayo hatima ya mataifa dhaifu inapaswa kuainishwa. Amesema, katika Siku ya Kimataifa ya Quds inapaswa kuyafahamisha madola ya kibeberu kwamba, hayawezi kufanya ubeberu wao katika nchi za Kiislamu. Ijumaa ya mwisho ya kila mwezi mtukufu wa Ramadhani ilitangazwa na mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hayati Imam Ruhullah Khomeini kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Quds na akawataka Waislamu kote duniani kushiriki kwenye maandamano ya siku hiyo kwa ajili ya kutetea kibla chao cha kwanza na Waislamu wenzao wanaoendelea kukandamizwa na utawala katili wa Israel huko Palestina.

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)