Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 01 Julai 2015 09:39

Araki: Siku ya kimataifa ya Quds iwe ya hamasa

Araki: Siku ya kimataifa ya Quds iwe ya hamasa

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bait amewaandikia barua maulamaa na wanazuoni katika ulimwengu wa Kiislamu akiwataka kuwahamasisha Waislamu washiriki kwa wingi katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds.

Katika barua hiyo, Ayatullah Muhsin Araki ameashiria fitina zinazofanywa na mabeberu dhidi ya Waislamu na kuandika kuwa: Njama zinazofanywa na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel kwa shabaha ya kuwaweka mbali Waislamu na thamani na malengo yao zimekuwa sababu ya kutokea hitilafu, mauaji ya kizazi na watoto na kudhoofika jamii za Waislamu. Ameongeza kuwa inasikitisha kuona kwamba, wanaoeneza hitilafu hizo ni Waislamu majahili.

Sehemu moja ya barua ya Katibu Mkuu wa Jumuya ya Kimataifa ya Ahlul Bait imesema: Ugaidi na kundi la kigaidi la Daesh katika nchi za Iraq na Syria, hali ya kusikitisha ya Yemeni na hitilafu zilizopo katika nchi za Kiislamu havipaswi kuwa sababu ya kusahauliwa malengo makuu ya Umma wa Kiislamu kama Palestina na Quds Tukufu. Amesema Palestina daima imekuwa sababu ya umoja na mshikamano wa Kiislamu na kwamba katika Siku ya Kimataifa ya Quds kutadhihirika zaidi umoja na mshikamano huo wa Umma wa Kiislamu kwa juhudi za maulamaa za kuuzindua Umma na kuweka wazi njama za Wazayuni na Marekani.

Ijumaa ya mwisho ya kila mwezi mtukufu wa Ramadhani ilitangazwa na mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hayati Imam Ruhullah Khomeini kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Quds na akawataka Waislamu kote duniani kushiriki kwenye maandamano ya siku hiyo kwa ajili ya kutetea kibla chao cha kwanza na Waislamu wenzao wanaoendelea kukandamizwa na utawala katili wa Israel huko Palestina.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)