Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Alkhamisi, 18 Juni 2015 21:53

HAMAS yawataka Waislamu kuuhami mji wa Quds

HAMAS yawataka Waislamu kuuhami mji wa Quds

Mjumbe maalum wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) nchini Lebanon ametoa mwito kwa nchi za Kiislamu kuuhami mji mtakatifu wa Quds pamoja na kuvunja mzingiro wa kidhalimu wa Wazayuni dhidi ya eneo la Gaza. Ali Baraka amesema kuwa, utawala haramu wa Israel unalenga kuuyahudisha mji wa Quds na kwa mantiki hiyo kuna haja ya kuchukuliwa hatua za kivitendo kuulinda mji huo mtakatifu unaobeba masjidul Aqsa ambao ni qibla cha kwanza cha Waislamu. Baraka ametoa mkono wa tahania kwa Waislamu kwa mnasaba wa kuanza mwezi mtukufu wa Ramadhani na kuwataka kuwakumbuka wananchi madhulumu wa Palestina kupitia dua ndani ya mwezi huu mtukufu. Ali Baraka amesema HAMAS itaendelea kutetea maslahi ya Wapalestina hadi pale wakimbizi wote watakaporejea kwenye ardhi zao zilizoporwa na utawala haramu wa Israel.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)