Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 02 Juni 2015 21:43

Israel yatenga mamilioni ya dola kuiyahudisha Quds

Israel yatenga mamilioni ya dola kuiyahudisha Quds

Katibu wa Baraza la Kiislamu na Kikristo la kuilinda Quds na matukufu ya Palestina amesema utawala wa Kizayuni wa Israel umetenga mamilioni ya dola kwa madhumuni ya kuuyahudisha mji mtakatifu wa Baitul Muqaddas. Hana Issa amesema utawala wa Kizayuni umetenga bajeti ya dola milioni 17 pamoja na kuandaa miswada ya sheria sita mipya inayosubiri kupasishwa kwenye bunge la utawala huo haramu la Knesset kwa ajili ya kuiyahudisha Quds Tukufu. Katibu wa Baraza la Kiislamu na Kikristo la kuilinda Quds na matukufu ya Palestina amesisitiza kuwa ili kufuta athari za Kiislamu na Kiarabu za Quds, utawala wa Kizayuni unatekeleza mpango hatari kabisa wa kuugawa msikiti mtukufu wa al Aqsa kimahali na kinyakati na kupiga marufuku walinzi wake kuingia msikitini humo. Aidha ametanabahisha kuwa hali katika mji mtukufu wa Quds unaokaliwa kwa mabavu ni ngumu mno na utawala wa Kizayuni unaitumia vibaya hali ya migogoro iliyozikumba nchi za Kiarabu na misimamo ya kindumakuwili inayoonyeshwa kimataifa kuhusiana na suala la Palestina. Wakati huohuo Sheikh Muhammad Hussein, mufti wa Quds na Palestina amesema msikiti wa al Aqsa ni milki ya Waislamu na ni wajibu kwa Waislamu wote na Wakristo kusimama imara na kukabiliana na njama za utawala wa Kizayuni za kutaka kubadilisha sura ya mji wa Quds…./

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)