Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 11 Disemba 2015 11:31

AP: Saudia inaficha idadi halisi ya waliouawa Mina

AP: Saudia inaficha idadi halisi ya waliouawa Mina

Uchunguzi wa hivi karibuni umebaini kuwa idadi ya mahujaji waliopoteza maisha katika maafa ya Mina wakati wa Ibada ya Hija ni mara tatu zaidi ya takwmu rasmi zinazotangazwa na watawala wa Saudia.

Shirika la Habari la Associated Press limesema limefanya uchunguzi na kubaini kuwa tokea Septemba 26 wakati wa maafa ya Mina, Saudia haijabadili takwimu zake rasmi zilizoonyesha ni watu 769 ndio waliopoteza maisha katika maafa hayo yaliyojiri wakati wa Sikukuu ya Idul Adh'ha. AP imesema uchunguzi wake umebaini kuwa kwa uchache, Mahujaji 2,411 walipoteza maisha katika maafa hayo. Takwimu hizo ni kwa msingi wa taarifa za vyombo vya habari na takwimu rasmi za nchi 36 kati ya 180 zilizotuma mahujaji katika ibada ya Hija mwaka huu. Iran ni nchi iliyoathiriwa zaidi katika maafa hayo baada ya raia wake 460 kupoteza maisha katika tukio hilo la kusikitisha. Shirika la Hija la Iran linasema uchunguzi wake umebaini kuwa mahujaji zaidi ya 4,700 walipoteza maisha Mina huku baadhi ya duru zikiitaja idadi hiyo kuwa ni 7,000. Imedokezwa kuwa moja ya sababu ya Saudia kuficha ukweli kuhusu waliopoteza maisha Mina ni kujaribu kulinda itibari ya Mrithi wa Kiti cha Ufalme Mohammad bin Nayef ambaye ndie msimamizi wa Ibada ya Hija. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeilaumu Saudia kwa usimamizi mbovu wa ibada ya Hija na kutoa wito wa nchi za Kiislamu kushirikishwa katika uandaaji wa ibada hiyo ya kila mwaka ya Waislamu.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)