Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 25 Novemba 2015 19:46

Mwili wa balozi wa zamani wa Iran kurejeshwa kesho

Mwili wa balozi wa zamani wa Iran kurejeshwa kesho

Mwili wa Ghazanfar Roknabadi, balozi wa zamani wa Iran nchini Lebanon ambaye alikuwa miongoni mwa mahujaji waliotoweka katika maafa ya Mina utarejeshwa nchini kesho baada ya kutambuliwa. Mortaza Roknabadi, ndugu wa balozi huyo wa zamani wa Iran nchini Lebanon amethibitisha habari ya kufariki dunia kaka yake katika maafa ya Mina na kueleza kwamba baada ya ufuatiliaji uliofanywa, mwili wa Ghazanfar Roknabadi utasafirishwa na kurejeshwa nchini hapo kesho. Aidha amesema familia ya Roknabadi inafuatilia kisheria tukio hilo ambalo kwa mtazamo wa wataalamu wengi ni la kutia shaka na kusisitiza kwamba Saudia inapaswa kuwajibika kuhusiana na maafa ya Mina. Mahujaji 464 wa Kiirani walifariki dunia tarehe 24 Septemba mwaka huu katika Siku ya Idul-Adh’ha wakati walipokuwa wakitekeleza amali za Hija katika ardhi ya Mina kwenye mji mtukufu wa Makka. Hatima ya mahujaji wengine kadhaa wa Kiirani waliotoweka katika tukio hilo bado haijajulikana.

Wakati huohuo Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa aliyeko mjini Tehran amesema umoja huo unaunga mkono ufuatiliaji unaofanywa na Iran kuhusiana na maafa ya Mina. Gary Lewis, ameyasema hayo leo katika mazungumzo na Amir Mohsen Ziaee, Mkuu wa Shirika la Hilali Nyekundu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kueleza kuwa Hilali Nyekundu ya Iran imekuwa ikitoa ushirikiano kila mara kwa Umoja wa Mataifa katika ufanyaji tathmini wa operesheni wakati zinapotokea ajali na katika shughuli za utoaji misaada ya kibinadamu…/

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)