Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 22 Novemba 2015 11:43

Uzembe wa Saudia ulipelekea kufa mahujaji Mina

Uzembe wa Saudia ulipelekea kufa mahujaji Mina

Mkuu wa Taasisi ya Hija na Ziara ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, mahujaji waliopoteza maisha yao katika maafa ya Mina katika ibada ya Hija mwaka huu wamekuwa wahanga wa uzembe wa watawala wa ukoo wa Aal-Saud. Said Ohadi amesema hayo katika kongamano la kuwakumbuka wahanga wa maafa ya Mina na kusisitiza kwamba, ibada ya Hija kutokana na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya watu, inahitaji kuchukuliwa hatua za maana na makini katika kusimamia ibada hiyo na kuhakikisha usalama wa roho na maisha ya mahujaji wa nyumba ya Mwenyezi Mungu. Mkuu wa Taasisi ya Hija na Ziara ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alinukuliwa hivi karibuni akisema kuwa, hatima ya mahujaji wa Iran waliopotea katika maafa ya Mina itajulikana kikamilifu wiki ijayo. Mwaka huu Iran ilituma mahujaji 64 elfu nchini Saudi Arabia na mahujaji 465 walipoteza maisha kwenye maafa ya Mina yaliyotokea tarehe 24 Septemba, siku ya sikukuu ya Idul Adh'ha. Kwa mujibu wa vyanzo vya Wizara ya Afya ya Saudi Arabia, zaidi ya mahujaji 7,000 walipoteza maisha yao katika maafa ya Mina yaliyotokea katika ibada ya Hija mwaka huu.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)