Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 21 Novemba 2015 05:04

Maiti zaidi za Watanzania maafa ya Mina zatambuliwa

Maiti zaidi za Watanzania maafa ya Mina zatambuliwa

Wizara ya Mashauri ya Kigeni na Ushirikiano wa Kimataifa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza kuwa, maiti nyingine nne za mahujaji wa nchi hiyo ambao hatima yao ilikuwa haijulikani baada ya maafa ya Mina huko Saudia katika ibada ya Hija mwaka huu zimetambuliwa. Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali cha Wizara ya Mashauri ya Kigeni na Ushirikiano wa Kimataifa imeeleza kuwa, mahujaji wengine wanne kutoka Tanzania ambao walikuwa miongoni mwa wale waliokuwa hawajulikani waliko tangu yalipotokea maafa ya Mina Septemba 24 mwaka huu wametambuliwa kuwa miongoni mwa mahujaji waliofariki dunia. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, majina ya mahujaji hao kutoka taasisi ya Hija ya Khidmat al-Islamiyyah ni Abdul Idd Hussein, Adam Abdul Adam, Rashida Adam Abdul na Khadija Abdukhalik Said.

Kutambuliwa kwa maiti za mahujaji hao kunaifanya idadi ya mahujaji wa Tanzania walipoteza maisha katika mkanyagano wa Mina Saudi Arabia kufikia 32. Aidha hadi sasa mahujaji saba kutoka Tanzania bado hatima yao haijulikani na jitihada za kuwatafuta zinaendelea. Kwa mujibu wa vyanzo vya Wizara ya Afya ya Saudi Arabia, zaidi ya mahujaji 7,000 walipoteza maisha yao katika maafa ya Mina yaliyotokea katika ibada ya Hija mwaka huu.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)