Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 20 Novemba 2015 11:07

Hatima ya mahujaji wa Iran Mina kujulikana wiki ijayo

Hatima ya mahujaji wa Iran Mina kujulikana wiki ijayo

Mkuu wa Taasisi ya Hija na Ziara ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, hatima ya mahujaji wa Iran waliopotea katika maafa ya Mina itajulikana kikamilifu wiki ijayo.
Shirika la habari la IRNA limemnukuu Bw. Said Ohadi akisema hayo na kuongeza kuwa, kwa mujibu wa mazungumzo yaliyofanyika baina ya Iran na Saudi Arabia, hatima ya mwisho ya mahujaji hao wa Kiirani itajulikana wiki ijayo.
Ohadi ameongeza kuwa, kuna mahujaji 17 wa Kiirani hawajajulikana hatima yao hadi hivi sasa na kwamba watu wawili wa familia za mahujaji waliopotea huko Mina watatumwa nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kuchukuliwa vipimo vya vinasaba (DNA) ili kujua hatima ya jamaa zao.
Mwaka huu Iran ilituma mahujaji 64 elfu nchini Saudi Arabia na mahujaji 465 wamepoteza maisha kwenye maafa ya Mina yaliyotokea tarehe 24 Septemba, siku ya sikukuu ya Idul Adh'ha.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)