Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 09 Novemba 2015 19:51

Kadhi Palestina: Saudia ilisababisha maafa ya Mina

Kadhi Palestina: Saudia ilisababisha maafa ya Mina

Shakhsia mbalimbali wa Palestina wamewataja viongozi wa Saudi Arabia kuwa wahusika wakuu wa tukio la maafa ya Mina nchini humo. Abu Shahir al-Sheryani, kadhi wa Palestina sambamba na kuashiria maafa ya maelfu ya mahujaji wa nyumba ya Mwenyezi Mungu katika ibada ya kumpiga mawe shetani katika hija ya mwaka huu hapo tarehe 24 Septemba, amesema kuwa kitendo cha polisi ya Saudia kuwazuia mahujaji kutumia njia kuu na baadhi ya vichochoro, kilikusudiwa kuwaua wageni hao wa Mwenyezi Mungu. Aidha ameashiria joto kali lililokuwepo katika msimu huo wa Hija na pia msongamano mkubwa wa mahujaji katika kutekeleza ibada hiyo eneo la Mina na kuongeza kuwa, mbali na kushindwa kuboresha mazingira ya miundombinu, maafisa wa polisi wa Saudia walifeli pia kwa kiasi kikubwa katika kuwaongoza mahujaji, suala ambalo lilichangia kuibuka maafa hayo ya kihistoria. Kwa upande wake Abu Radhi al-Shakhshir, mmoja wa maulama wa Palestina, amekosoa vikali muamala mbaya wa polisi wa utawala wa Aal-Saud kwa mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu na kusema kuwa, polisi hao hawakuwa wakitoa msaada wowote kwa wageni hao wa Nyumba ya Allah licha ya kwamba miongoni mwao walikuwamo watu wa umri mkubwa. Naye kwa upande wake Ziyad al-Hamudi, mkuu wa kituo cha haki za kijamii eneo la Quds, Palestina sambamba na kubainisha kwamba, Saudia inamiliki suhula nyingi kwa ajili ya kuendesha ibada ya Hija, amesema kuwa ilitazamiwa kuwa Aal-Saud wangesimamia vyema ibada ya Hija sanjari na kuwadhaminia usalama na amani mahujaji hao tangu wanapowasili uwanja wa ndege hadi wanaporejea makwao, suala ambalo halikutekelezwa kabisa. Kwa mujibu wa vyanzo vya Wizara ya Afya ya Saudia, zaidi ya mahujaji 7000 walipoteza maisha yao katika tukio la Mina.  

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)