Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 09 Novemba 2015 09:17

Ohadi: Iran inafuatilia vilivyo Wairani waliopotea Mina

Ohadi: Iran inafuatilia vilivyo Wairani waliopotea Mina

Saeed Ohadi Mkuu wa Taasisi ya Hija na Ziara ya Iran amesema kuwa kujulikana hatima ya mahujaji wa Kiirani waliopotea katika maafa ya Mina wakati wa ibada ya Hija mwaka huu huko Saudi Arabia, ni miongoni mwa matakwa makuu ya Iran kwa viongozi wa Saudia. Ohadi amesema kuwa mahujaji 25 wa Iran hadi sasa hawajulikani walipo. Mkuu wa Taasisi ya Hija na Ziara ya Iran amesema, akiwa ziarani hivi karibuni nchini Saudia, kuwa vinasaba yaani DNA vya mahujaji wa Iran waliopotea vilikabidhiwa kwa maafisa wa Saudi Arabia na kwamba maafisa hao wanataraji kutangaza matokeo ya uchunguzi wao katika muda wa siku kumi zijazo.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)