Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 08 Novemba 2015 13:23

Masufi Misri: Mfalme Salman alihusika maafa ya Mina

Masufi Misri: Mfalme Salman alihusika maafa ya Mina

Katibu mkuu wa Jumuiya ya makundi ya Kisufi nchini Misri, amemtaja Salman bin Abdulaziz Al Saud, mfalme wa Saudia kuwa muhusika mkuu wa maafa ya hija ya mwaka huu. Abdullah al-Nasser amesema kuwa matukio ya kuumiza ya ibada ya hija ya mwaka huu hayakuwa ya kawaida, na kwamba mfalme huyo wa Saudia ndiye mbeba dhima mkuu wa maafa ya Mina na kuanguka kwa winchi katika haram ya Makkah. Al-Nasser amesisitiza kuwa, kwa kuzingatia kuwa mahujaji wamepoteza maisha kwa uzembe na katika mamlaka ya mtawala huyo, hivyo kuna udharura wa Mfalme Salman kushtakiwa katika vyombo vya sheria na kuwajibishwa kwa jinai hizo. Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Makundi ya Kisalafi nchini Misri ameongeza kuwa, sababu ya kujiri maafa ya ibada ya hija ya mwaka huu, ni kupenda kujitanua utawala wa Aal-Saud katika ibada hiyo takatifu, hususan kufuatia watawala hao kukataa msaada wa nchi nyingine za Kiislamu na kujitwisha jukumu la usalama wa mahujaji wao wenyewe. Akiashiria pato kubwa la fedha inalolipata Saudia kutokana na ibada hiyo ya hija amesema kuwa, utawala wa Aal- Saud unatilia maanani suala la fedha pekee unazoingiza kila mwaka kutoka kwa mahujaji, lakini hauko tayari kuwadhaminia usalama mahujaji hao.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)