Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 02 Novemba 2015 13:44

"Hatima ya mahujaji waliotoweka inapasa kuwekwa wazi"

"Hatima ya mahujaji waliotoweka inapasa kuwekwa wazi"

Muhammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa Saudi Arabia inapaswa kubainisha hatima ya mahujaji wengine waliotoweka katika maafa ya Mina kwenye ibada ya Hija mwaka huu, na kwamba Iran inasubiri kurejea nchini Balozi wa zamani wa Iran mjini Beirut Lebanon Qazanfar Roknabadi ambaye ni miongoni mwa mahujaji wasiojulikana walipo. Zarif amesema kuwa, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran na familia ya balozi Roknabadi wanasubiri kurejea balozi huyo na kwamba Iran inataraji kuwa hatima ya mwanadiplomasia huyo itawekwa wazi siku si nyingi. Muhammad Javad Zarif ameyasema hayo jana hapa Tehran akihutubia mkutano wa mabalozi na wakuu wa ujumbe wa kidiplomasia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nje ya nchi. Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, lengo kuu zaidi la chombo cha udiplomasia cha Iran ni kuhakikisha kuwa mahujaji wa Kiirani ambao kila mwaka huelekea Saudia kwa ajili ya amali tukufu ya Hija, wanakwenda na kurejea katika ziara hiyo ya kimaanawi kwa amani na usalama.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)