Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 27 Oktoba 2015 07:20

Kamati ya kufuatilia maafa ya Mina kuundwa

Kamati ya kufuatilia maafa ya Mina kuundwa

Mkuu wa Taasisi ya Ziara na Hija ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amearifu juu ya kuundwa kamati ya kufuatilia maagizo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu maafa ya Mina. Saeed Ohadi alisema jana katika mkutano na vyombo vya habari hapa Tehran kuwa, kikao cha kwanza cha kamati ya kufuatilia maagizo yaliyotolewa na Ayatullahil udhma Sayyid Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu maafa ya Mina kitafanyika Jumatano wiki hii. Ohadi ameashiria kuwepo kwenye kamati hiyo kundi la wahadhiri wa Vyuo Vikuu na wanaharakati katika ngazi ya kimataifa na kubainisha kuwa, kamati hiyo ina mpango wa kuainisha ramani ya njia, kwa kustafidi na uwezo na suhula za taasisi za kimataifa, za haki za binadamu na za kiraia ili kuzuia kukaririwa maafa kama ya Mina. 

Mkuu wa Taasisi za Ziara na Hija ya Iran pia ameashiria kuhusu safari yake ya Jumamosi wiki ijayo nchini Saudia kwa ajili ya kushiriki katika Kikao cha Nne cha Kamati ya Pamoja yaani kikao cha uhitimishaji, na kuongeza kuwa, hadi sasa hakuna taarifa zozote zilizotolewa kuhusu hatima ya mahujaji 36 wa Iran waliotoweka katika ibada ya Hija mwaka huu.  

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)