Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 26 Oktoba 2015 09:13

“Nchi za Kiislamu ziijue sababu ya maafa ya Mina”

“Nchi za Kiislamu ziijue sababu ya maafa ya Mina”

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametaka kuweko mazungumzo kati ya nchi zote za Kiislamu ili kuweza kujua sababu zilizopelekea kutokea maafa ya Mina nchini Saudi Arabia.

Mohammad Javad Zarif alisema hayo wakati alipompokea balozi mpya wa Mali aliyekwenda kujitambulisha kwake.

Ametoa mkono wa pole kwa serikali na wananchi wa Mali kutokana na kupoteza maisha mahujaji wa nchi hiyo katika maafa ya Mina na kuelezea matumaini yake kwamba nchi zote za Kiislamu zitafanya juhudi za pamoja za kutafuta sababu za maafa hayo na kuzuia yasitokee tena katika siku za usoni.

Kwa upande wake, balozi wa Mali hapa mjini Tehran ameelezea wasiwasi wake kutokana na kuongezeka vitendo vya kigaidi katika maeneo tofauti duniani na ameitaka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ishirikiane na nchi yake katika kupambana na vitendo hivyo nchini humo.

Aidha amegusia mwafaka wa nyuklia uliofikiwa kati ya Iran na kundi la 5+1 na kusema kuwa huo ni ushindi mkubwa na kumwalika Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran atembelee nchi yake.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)