Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 23 Oktoba 2015 12:40

Waislamu Niger wailaumu Saudia kwa maafa ya Mina

Waislamu Niger wailaumu Saudia kwa maafa ya Mina

Muungano wa taasisi za Kiislamu nchini Niger zimekosoa vikali udhaifu wa Saudia wa kushindwa kusimamia ipasavyo ibada ya Hija na kusababisha maafa ya maelfu ya mahujaji wa nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu. Taarifa iliyotolewa na muungano huo unaoundwa na taasisi 30 za Kiislamu imesema kuwa, ni suala la kusikitisha mno kwa utawala wa Saudia kushindwa kabisa kuwadhaminia usalama mahujaji ambapo kila mwaka kumekuwa kukishuhudiwa maafa na visa mbalimbali vya ukosefu wa usalama kwa wageni hao wa Mwenyezi Mungu. Ripoti hiyo pia imesisitiza kuwa, udhaifu na uzembe wa makusudi wa maafisa wa Aal Saud, ndio uliosababisha maafa makubwa ya eneo la Mina. Aidha umoja wa taasisi hizo umewataka Waislamu kote duniani kuushinikiza utawala wa Saudia kuruhusu kupewa usaidizi katika usimamizi wa ibada hiyo ya Hija ili kuzuia kujikariri kwa matukio hayo. Hii ni katika hali ambayo Khalifa Tijani, ambaye ana wafuasi zaidi ya milioni 17 ndani na nje ya Niger na mwakilishi maalumu wa tume ya viongozi 20 wa twariqa ya Tijani, aliwasili ubalozi wa Iran mjini Niamey, kwa ajili ya kutoa rambirambi kwa maafa ya mahujaji wa maafa ya Mina. Zaidi ya mahujaji 5000, wanasadikiwa kupoteza maisha katika tukio la mkanyagano lililotokea kufuatia msafara wa ufalme wa Saudia kwenye kwenye eneo hilo na kupelekea kufungwa njia kuu katika sikukuu ya Mfunguo Tatu, Idul Adh'ha na kusababisha msongamano mkubwa mahujaji waliokosa njia ya kutokea.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)