Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Alkhamisi, 22 Oktoba 2015 19:25

Mali imepoteza mahujaji wengi katika maafa ya Mina

Mali imepoteza mahujaji wengi katika maafa ya Mina

Serikali ya Mali imetangaza kuwa, inaongoza kwa kupoteza raia wake wengi katika tukio chungu la maafa ya Mina, Saudia mwezi uliopita, ikilinganishwa na nchi nyingine za Kiafrika. Suisse Fatoumata Kuyateh, mkuu wa mashirika ya safari na utalii nchini Mali na mmoja wa viongozi wa tume ya kukabiliana na majanga nchini humo, amesema kuwa kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa siku ya Jumanne, jumla ya mahujaji 282 wa Mali walifariki dunia katika tukio la mkanyagano lililojiri hapo tarehe 24 mwezi uliopita katika ibada ya kumpiga mawe shetani eneo la Mina, Saudia. Aidha afisa huyo ameongeza kuwa, hadi sasa mahujaji wengine 87 hawajulikani walipo. Kwa utaratibu huo, Mali ndio nchi ya kwanza kati ya nchi za Kiafrika iliyopoteza raia wake wengi katika tukio hilo. Aidha Fatoumata ameongeza kuwa, umoja wa mashirika ya safari na utalii nchini humo kwa kushirikiana na serikali, umeunda idara ya ushauri wa kisaikolojia itakayosimamiwa na Wizara ya Masuala ya Dini na Tamaduni kwa lengo la kutoa ushaurinasaha kwa familia za wahanga wa maafa hayo. Kabla ya hapo idadi ya mahujaji wa Mali walioarifiwa kupoteza maisha ilikuwa ni 198. Zaidi ya mahujaji 5000, wanasadikiwa kupoteza maisha katika tukio la mkanyagano huo, lililotokea kufuatia msafara wa Mohammad Bin Salman Al Saud, mrithi wa kiti cha ufalme na Waziri wa Ulinzi wa Saudia, kuwasili eneo la Mina siku ya Iddil-Adh’ha, huku akiandamana na mamia ya askari wake wanaomlinda, kabla ya kufunga njia kuu ya kuingilia eneo hilo, suala ambalo lilisababisha mahujaji kukosa njia ya kutokea na hivyo kukanyagana na kupoteza maisha.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)