Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 20 Oktoba 2015 19:56

Zarif: Saudia haikuwajibika katika maafa ya Mina

Zarif: Saudia haikuwajibika katika maafa ya Mina

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema leo kuwa, tunaamini kwamba serikali ya Saudi Arabia na maafisa wanaosimamia Hija nchini humo hawakuwajibika na hawakutekeleza majukumu yao kuhusiana na maafa ya Mina, hawakuchukua hatua zinazofaa kwa ajili ya kuokoa roho za mahujaji na wala hawakutoa huduma zinazopasa kwa mahujaji waliokwama kwenye maafa hayo.
Dk Mohammad Javad Zarif ameongeza kuwa, ni jambo la kusikitisha kuona kuwa Waislamu wengi kutoka nchi tofauti za dunia wamepoteza maisha yao katika maafa ya Mina. Ameongeza kuwa: Wizara ya Mambo Nje ya Iran imekuwa ikifuatilia kwa karibu suala hilo tangu mwanzoni mwa maafa hayo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa mahujaji wote wa Iran wanarejea nchini wakiwa salama usalimini.
Amesema, Tehran inaendelea kufuatilia suala la kurejeshwa nyumbani miili iliyobakia ya mahujaji wa Iran. Aidha amesema, juhudi nyingine zinazofanywa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ni kuhakikisha kuwa hatua za maana zinachukuliwa kwa ajili ya kuzuia kutokea tena maafa kama ya Mina.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)