Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 19 Oktoba 2015 13:02

Kodivaa: Raia wetu zaidi ya 52 walifariki dunia Mina

Kodivaa: Raia wetu zaidi ya 52 walifariki dunia Mina

Duru rasmi nchini Kodivaa zimetangaza idadi ya raia wa nchi hiyo waliopoteza maisha yao katika tukio chungu la Mina, Saudi Arabia hapo tarehe 24 Septemba mwaka huu. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kwa akali watu 52 raia wa Ivory Coast walipoteza maisha katika tukio hilo. Messamba Bamba, mkuu wa masuala ya kidini nchini humo amesema kuwa awali idadi ya wahanga wa maafa ya Mina ilikuwa ni watu 14 pekee na kwamba idadi hiyo imeongezeka na kufikia 52. Aidha ameongeza kuwa, idadi hiyo sio ya mwisho kwani bado kuna watu saba ambao hadi sasa hawajulikani walipo. Hii ni katika hali ambayo kwa mujibu wa Bamba, watu 120 walijeruhiwa katika tukio hilo. Kufuatia hali hiyo, Rais Alassane Ouattara wa nchi hiyo ametoa mkono wa pole kwa familia za wahanga, ametangaza tarehe 24 ya mwezi huu kuwa ni siku ya maombolezo ya kitaifa nchini humo. Hatua hiyo imekuja kufuatia serikali ya Yamoussoukro kutuma ujumbe maalumu nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kufuatilia hatima ya raia wake ambao walipoteza maisha kwenye maafa hayo ya Mina. Tukio chungu la Mina, lilijiri baada ya maafisa wa Saudia kufunga njia kuu ya kuelekea eneo ili kupisha msafara wa kifalme kuingia eneo hilo. Mahujaji wanaokadiriwa 5000, wamepoteza maisha yao kwenye maafa hayo.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)