Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 18 Oktoba 2015 14:11

Zaidi ya Mahujaji 5,000 waliofariki Mina wazikwa Makka

Zaidi ya Mahujaji 5,000 waliofariki  Mina wazikwa Makka

Mkuu wa Taasisi ya Hija na Ziara ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuna Mahujaji zaidi ya elfu 5 waliopoteza maisha katika maafa ya Mina ambao wamezikwa katika mji mtakatifu wa Makka nchini Saudi Arabia. Saeed Ohadi amesema hayo baada ya kurejea hapa nchini akitokea Saudia ambapo akiwanukuu viongozi wa utawala wa Aal Saud amebainisha kuwa, Mahujaji zaidi ya elfu tano waliopoteza maisha katika msongamano wa Mina wamezikwa katika makaburi ya mashahidi mjini Makka. Ameongeza kuwa, kwa mujibu wa matamshi ya viongozi wa Saudia katika kikao cha pamoja ni kuwa, idadi ya Mahujaji waliopoteza maisha katika maafa ya Mina imepindukia elfu sita. Mkuu wa Taasisi ya Hija na Ziara ya Iran ameeleza kuwa, kuvitambua viwiliwili vya Mahujaji wa Kiirani baina ya idadi hiyo ilikuwa kazi ngumu mno. Aidha amesema kuwa, kuna Mahujaji 29 wa Iran waliofariki dunia katika maafa ya Mina ambao wamezikwa pasina ya serikali ya Iran kupewa taarifa; hata hivyo mahala walipozikwa panajulikana, makaburi yao yanafahamika na walizikwa kwa kuzingatia taratibu zinazotakiwa. Hadi sasa kuna Mahujaji 36 wa Kiirani ambao hatima yao bado haijajulikana na tayari imeundwa kamati maalumu ya pande mbili kwa ajili ya kufuatilia kadhia hiyo.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)