Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 18 Oktoba 2015 09:23

“Kuna udharura wa maafa ya Mina kuchunguzwa"

“Kuna udharura wa maafa ya Mina kuchunguzwa"

Mshauri wa Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) katika masuala ya kimataifa amesema kuwa, kuna haja ya kufanyika uchunguzi wa pande zote kuhusiana na maafa ya Mina yaliyopelekea maelfu ya Mahujaji kupoteza maisha katika ibada ya Hija mwaka huu. Hussein Sheikh al-Islam amesema kuwa, utendaji mbaya, usimamizi mbovu na kutokuwa na ustahiki ni miongoni mwa sifa za utawala wa Aal Saud nchini Saudi Arabia. Mshauri wa Spika wa Bunge la Iran katika masuala ya kimataifa ameongeza kuwa, usimamizi dhaifu na utendaji mbovu ambao chimbuko lake ni Uwahabi umekuwa ukionekana katika hatua za ndani na nje zinazochukuliwa na utawala wa Aal Saud. Sheikh al-Islam amebainisha kuwa, mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu nchini Iran unafuatilia kwa nguvu zake zote maafa ya Mina. Amesisitiza kuwa, kuundwa kamati ya kutafuta ukweli kuhusu maafa ya Mina ni haki ya familia zilizopoteza ndugu zao katika maafa hayo. Saudia imeendelea kukosolewa kieneo na kimataifa kutokana na kupoteza maisha maelfu ya Mahujaji katika msimu wa Hija mwaka huu.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)