Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 30 Machi 2016 14:27

Iran yamaliza hatua ya makundi kuelekea Kombe la Dunia 2018

Iran yamaliza hatua ya makundi kuelekea Kombe la Dunia 2018

Timu ya taifa ya soka ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetinga hatua ya mwisho ya mbio za kusaka nafasi ya kucheza Kombe la Dunia mwaka 2018. Hii ni baada ya kuisasambua Oman mabao 2-0 katika mchuano wa Kundi D Jumanne katika uwaja wa taifa wa Azadi jijini Tehran.

Nyota wa mchezo huo alikuwa kiungo Sardar Azmoun ambaye alifunga mabao yote mawili kwa kichwa katika dakika ya 16 na 23.

Kwa ushindi huo, Iran inasalia kileleni mwa Kundi D ikiwa na pointi 20 na hivyo kujikatia tiketi ya kushiriki hatua ya mwisho ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018.

Itakumbukwa kuwa, timu ya taifa ya Iran iliichabanga India mabao 4-0 katika mchuano mwingine wa kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Dunia mwaka 2018.   

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …