Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Alkhamisi, 24 Machi 2016 20:10

Iran yatwaa Kombe la Mashindano ya Voliboli China

Iran yatwaa Kombe la Mashindano ya Voliboli China

Timu ya taifa ya wanaume ya voliboli ya kuketi chini ya jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetwaa Kombe la Dunia la Voliboli ya Walemavu nchini China. Katika kipute cha fainali kilichopigwa katika uwanja wa Inji mjini Hangzhou, timu ya Iran iliipeleka mchakamchaka Brazil na kuizaba seti tatu za mpigo za 25-20, 25-13 na 25-14 na kutwaa ubingwa wa mashindano hayo yajulikanayo kama World Paravolley Intercontinental Cup. 

Kiungo wa timu hiyo ya Iran ya Kiislamu, Davoud Alipourian aliteuliwa kuwa mchezaji bora mwenye thamani katika mashindao hayo ya dunia. Brazil ambayo iliibuka katika nafasi ya pili ililazimika kuridhika na medali ya fedha huku mabingwa wa Iran wakirudi nyumbani na dhahabu.

Timu ya taifa ya wanawake ya Iran katika mchezo huo iliibuka katika nafasi ya 5 siku ya Jumanne. Timu ya Marekani ndiyo iliyotwaa ubingwa wa mchezo huo wa upande wa wanawake baada ya kuichabanga mwenyeji China seti 3-1, za 25-22, 12-25, 25-20 na 28-26.

Mashindano hayo ya kimataifa ya voloboli ya walemavu yalianza Machi 17 na kufunga pazia lake Machi 23.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …