Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 14 Machi 2016 15:40

Soka: Mkufunzi wa Iran ataja kikosi cha taifa

Soka: Mkufunzi wa Iran ataja kikosi cha taifa

Mkufunzi mkuu wa timu ya taifa ya soka ya Iran, Carlos Queiroz amekiita kambini kikosi cha wachezaji 19, ili kuanza kukinoa kwa ajili ya michuano miwili ya kimataifa itakayopigwa karibuni hivi. Kikosi hicho kimetakiwa kuripoti mara moja katika Uwanja wa Taifa wa Azadi mjini Tehran, ili kujiandaa kwa michuano ya kimataifa dhidi ya India na Oman. Kikosi hicho kinajumuisha Omid Ebrahimi, Mohsen Karimi, Sajjad Shahbazzadeh (Esteghlal FC), Ali Ashouri (Esteghlal ya Khuzestan),  Sousha Makani, Ahmad Nourollahi, Kamal Kamyabinia, Mehdi Taremi, Ramin Rezaian, Farshad Ahmadzadeh, Mohammad Ansari (Persepolis), Mehrdad Mohammadi (FC Rah-ahan), Mehdi Torabi (FC Saipa), Darioush Shojaian (Gostaresh ya Tabriz), Ezzatollah Pourghaz, Mohammad Hossein Kan’ani (Malavan ya Anzali), Seyed Jalal Hosseini, Vahid Amiri, na Alireza Beiranvand (FC Naft yaTehran). Aidha Kamati ya Ufundi wa timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Iran imeandaa orodha yake yenye wachezaji 16, ambayo wana nafasi kubwa ya kujumuishwa katika orodha ya mwisho ya kikosi hicho cha soka cha Iran. Orodha hiyo inawajumuisha wachezaji wengi wa Iran wanaokipiga nje ya nchi. Wachezaji hao ni pamoja Pejman Montazeri  (Al-Ahli ya Qatar), Masoud Shojaei (Al-Ghorafa ya Qatar), Ashkan Dejagah (Al-Arabi ya Qatar), Morteza Pouraliganji (As-Sad ya Qatar), Alireza Jahanbakhsh ( AZ Alkmaar ya Uholanzi), Ghoochan Nejhad  (Charlton Athletic), Milad Mohammadi (Terek Grozny, Russia), Karim Ansarifard (Panionios FC, Ugiriki), Sardar Azmoun, Saeid Ezzatollahi (Rostov, Russia), Ehsan Hajsafi (FSV Frankfurt, Ujerumani), Mohammad Reza Akhbari (Tractorsazi FC ya Iran), Mohammad Rashid Mazaheri, Ehsan Pahlavan (FC Zobahan ya Iran), Wouriya Ghafouri (FC Sepahan ya Iran) na Alireza Haghighi (Maritimo ya Ureno).

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …