Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 11 Machi 2016 05:44

Mwanamasumbwi wa Iran akataa kuzipiga na mwenzake wa Israel, aungana na Wapalestina

Mwanamasumbwi wa Iran akataa kuzipiga na mwenzake wa Israel, aungana na Wapalestina

Mchezaji wa timu ya taifa ya ndondi ya Iran amekataa kupigana na mchezaji wa ndondi wa utawala haramu wa Israel katika mashindano ya kimataifa ya ndondi ya Njia ya Hariri yanayofanyika Baku nchini Azerbaijan akionyesha uungaji mkono wake kwa taifa linalodhulumiwa la Palestina

Katika mashindano hayo ya kimataifa ya ndondi yaliyoanza jana katika mji mkuu wa Jamhuri ya Azerbaijan, mwanamasumbwi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mas'ud Abdullahi anayezipiga katika uzani wa kilo 69 aligoma kupigana na mwanamasumbwi kutoka Israel akipinga jinai zinazofanywa na utawala huo dhidi ya raia wa Palestina na uungaji mkono wake kwa taifa hilo linalodhulumiwa.

Wanamichezo wa Iran na baadhi ya nchi za Kiislamu daima wamekuwa wakilitetea taifa la Palestina dhidi ya utawala haramu wa Israel katika medani mbalimbali za kimataifa kwa kugoma kucheza na wawakilishi wa utawala huo katili unaoendelea kuua raia wasio na hatia wa Palestina na kukalia kwa mabavu ardhi na nchi yao.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …