Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 27 Februari 2016 09:07

Gianni Infantino arithi mikoba ya Blattet Fifa

Gianni Infantino, Rais mpya wa Shirikisho la Kandanda Duniani (FIFA). Picha na Maktaba Gianni Infantino, Rais mpya wa Shirikisho la Kandanda Duniani (FIFA). Picha na Maktaba

Gianni Infantino raia wa Uswisi amechaguliwa kuwa Rais mpya wa Shirikisho la Kandanda Duniani FIFA na kurithi mikoba ya Sepp Blatter aliyeongoza shirikisho hilo kwa miaka mingi. Katibu huyo mkuu wa Fifa alipata kura 115 katika raundi ya pili ikiwa ni kura 27 zaidi ya mpinzani wake wa karibu Sheikh Salman bin Ibrahim al-Khalifa wa Bahrain ambaye kwa sasa ni rais wa Shirika la Soka barani Asia. Mwanamfalme Ali bin al-Hussein wa Jordan alikuwa wa tatu akiwa na kura nne. Jerome Champagne mwanadiplomasia wa Ufaransa aliambulia patupu baada ya kushindwa kupata hata kura moja. Tokyo Sexwale kutoka Afrika Kusini alijiondoa kabla ya kura kuanza kupigwa mjini Zurich.  Raundi ya kwanza ya upigaji kura ilishindwa kum’baini mshindi wa moja kwa moja. Wingi wowote wa kura[zaidi ya aslimia 50] katika raundi ya pili ya uchaguzi huo ulikuwa unaweza kumwezesha mgombea kutangazwa mshindi katika raundi ya pili. Infantino ni wakili mwenye umri wa miaka 45 kutoka eneo la Brig jimbo la Valais nchini Switzerland ,ikiwa ni eneo lililopo chini ya maili sita kutoka nyumbani kwa Blatter. Blatter ambaye aliliongoza shirikisho hilo tangu mwaka 1998 alijiondoa mwaka uliopita kabla ya kupigwa marufuku katika shughuli zozote za kandanda kwa kipindi cha miaka sita. Baada ya kutangazwa mshindi, Infantino aliwaambia wajumbe waliopiga kura kwamba hakuweza kujielezea kutokana na hisia alizokuwa nazo. Lakini aliwaambia wajumbe kwamba ”kwa pamoja wataweza kuirudisha sura halisi ya Fifa na heshima yake”.

 

Na Salum Bendera

 

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …