Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Alkhamisi, 04 Februari 2016 15:06

DRC yatinga fainali ya CHAN

DRC yatinga fainali ya CHAN

Timu ya taifa ya soka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iko njiani kutwaa kwa mara ya pili Kombe la Michuano ya Mataifa ya Afrika CHAN, inayoendelea kusakatwa nchini Rwanda. Hii ni baada ya kuigaragaza Guinea mabao 5-4 katika mikwaju ya penati katika mchuano wa nusu fainali uliopigwa jana Jumatano katika uga wa Amahoro mjini Kigali.

Bolingi Mpangi aliipa DRC bao la kwanza kunako dakika ya 102 baada ya mchuano wao kumalizika kwa sare  tasa katika muda wa ada. Hata hivyo Ibrahima Sory Sankhon alisawazisha mambo kwa bao la aina yake ndani ya sekunde za mwisho baada ya kuongezewa dakika 30 na timu hizo kulazimika kuingia katika mikwaju ya penati.

Mabao ya DRC katika mikwaju ya penati yalifungwa na Bolingi, Joel Kimwaki, Michel Mika, Elia Meschack, Doxa Gikanji huku Ricky Tulenge na Joyce Lomalisa wakipoteza.

Mabao ya Guinea yalifungwa na Sory Sankhon, Leo Camara na Aboubacar Bangoura, huku Muhamed Thiam, Sory bangoura na Mohamed Youla wakipoteza.

DRC sasa itatoa kijasho na mshindi mchuno mwingine wa nusu fainali hii leo, kati ya Mali na Kodivaa.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …