Chapisha ukurasa huu
Alkhamisi, 04 Februari 2016 14:34

Taekwondo: Marefarii wa Iran kuamua mashindano ya Afrika

Taekwondo: Marefarii wa Iran kuamua mashindano ya Afrika

Marefarii wawili raia wa Iran wameteuliwa kuwa waamuzi katika mashindano ya mchezo huo ya African Qualification Tournament nchini Morocco. Shirikisho la Taekwondo Duniani WTF limewateuwa Shahram Arbabi na Hafez Mahdavi wa Iran ya Kiislamu kuwa marefarii katika mashindano hayo ya kieneo mjini Agadir nchini Morocco kati ya Februari 5 na 7.

Ili kushiriki katika mashindano ya Olimpiki ya Rio nchini Brazil mwaka huu, sharti marefarii wa mchezo huo wakiwemo wa Kiirani wafanye maamuzi katika mashindano  kadhaa katika kona mbali mbali ya dunia, chini ya uangalizi wa shirikisho la WTF.

Kamati ya Marefarii ya Shirikisho la Taekwondo Duniani hatimaye itateuwa marefarii 29 watakaoshiriki katika Olimpiki ya Rio. Shahram Arbabi na Hafez Mahdavi wa Iran watatoa uamuzi katika mashindano ya taekwondo nchini Morocco, na kuamua wanataekwondo watakaoshiriki katika mashindano ya msimu wa joto ya Rio de Janairo nchini Brazil baadaye mwaka huu.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)