Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 23 Januari 2016 17:41

Mwendesha baiskeli wa Iran ashinda medali Japan

Mwendesha baiskeli wa Iran ashinda medali Japan

Hossein Jamshidiyan, bingwa wa mchezo wa kuendesha baiskeli wa Jamhuri ya Kiislamu wa Iran ameshinda medali ya fedha baada ya kuibuka wa pili katika duru ya 36 ya Mashindano ya Uendeshaji Baiskeli barani Asia mwaka huu 2016 mjini Izu nchini Japan.

Mwendesha baiskeli huyo wa Iran alimaliza katika nafasi ya pili  kwa kutumia sekunde 60.25 nyuma ya raia wa Kazakhstan ambaye aliibuka mshindi kwa kutumia sekunde 45.42.

Mwakilishi wa mwenyeji Japan katika mashindano hayo alimaliza katika nafasi ya tatu kwa kutumia sekunde 60.34 na kujishindia medali ya shaba.

Ujumbe wa wanaspoti 21 kutoka Iran ya Kiislamu unahudhuria mashindano hayo ya bara Asia.

Mashindano hayo ya kikanda ambayo yalianza Januari 19 yanatazamiwa kufunga pazia lake Januari 30.   

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …