Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 29 Aprili 2016 20:41

Magaidi washambulia msikiti Aleppo, Syria; waua watu

Magaidi washambulia msikiti Aleppo, Syria; waua watu

Makundi ya kigaidi na kitakfiri yameushambulia kwa mizinga mji wa Aleppo kaskazini mwa Syria na kuua makumi ya raia na kujeruhi wengine wengi.

Mapema leo Ijumaa magaidi hao wamelenga eneo lililoko kando a msikiti mkuu wa Malakhan katika medani ya 'Babul-Faraj' na makazi ya raia mkoani humo ambapo zaidi ya watu 33 wameuawa na zaidi ya wengine 165 kujeruhiwa. Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imelaani mauaji hayo na kumtaarifu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la umoja huo, kuhusiana na mashambulizi ya magaidi hao dhidi ya makazi ya raia mkoani Aleppo na baadhi ya miji ya mkoa wa Idlib. Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imetangaza kuwa, hujuma hizo zimefanywa na magaidi hao kufuatia amri ya moja kwa moja ya baadhi ya nchi zinazounga mkono vitendo hivyo vya kigaidi kwa lengo la kukwamisha mkataba wa makubaliano ya kusitisha vita nchini Syria. Imesema kuwa, lau kama si amri ya serikali za Uturuki, Saudia na Qatar, kamwe mauaji hayo dhidi ya raia wa kawaida yasingeendelea. Kabla ya hapo zaidi ya raia 300 waliuliwa na magenge ya kitakfiri mjini Aleppo na katika mji mdogo wa al-Zahraa siku chache zilizopita.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …