Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 27 Aprili 2016 11:36

Amir wa Kuwait: Usitishaji vita Yemen uheshimiwe

Amir wa Kuwait: Usitishaji vita Yemen uheshimiwe

Kiongozi wa Kuwait, Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah ametaka kuheshimiwa kikamilifu usitishaji vita nchini Yemen.

Al-Sabah ameyasema hayo alipokutana na ujumbe wa Yemen unaohudhuria mazungumzo ya amani nchini Kuwait ambapo amesisitizia udharura wa kuheshimiwa usitishaji vita huo Aidha katika mazungumzo hayo, kiongozi wa Kuwait ameelezea matarajio yake kwamba pande mbili zitafikia makubaliano ya kisiasa na kupatikana amani ya kudumu nchini Yemen. Kwa upande wake Muhammad Abdul Salam, kiongozi wa ujumbe wa Yemen huko Kuwait amesema kuwa, kufikiwa makubaliano kunahitajia kwanza ushiriki wa makundi yote kwenye mustakbali wa Yemen. Abdul Salam ameongeza kuwa, duru za mazungumzo hayo ni zenye umuhimu mkubwa kwa ajili ya kufikiwa amani nchini Yemen. Kadhalika kiongozi huyo wa ujumbe wa Yemen amesisitiza kuwa, kuendelea kwa ukiukaji wa makubaliano ya usitishaji vita kunakofanywa na Saudia kupitia mashambulizi ya anga ya ndege zake huko nchini Yemen, kutakuwa na taathira hasi katika mwenendo wa mazungumzo ya Kuwait. Kwa mara kadhaa sasa Saudia imekuwa ikikiuka makubaliano ya usitishaji vita kwa kuendeleza hujuma zake za kikatili nchini Yemen na hivyo kukwamisha mwenendo wa mazungumzo ya amani.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …